
NEWS/ UPDATES
Dar es Salaam, 9 Juni 2026
Mwenyekiti wa Jukwaa la Asasi za Kiraia za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR Regional Civil Society Forum), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mwalimu Nyerere Foundation (MNF), Mzee Joseph Warioba Butiku, amepokea ujumbe kutoka Forum of Parliaments of the International Conference on the Great Lakes Region (FP-ICGLR) katika kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo na kubainisha maeneo ya ushirikiano wa pamoja katika kukuza amani, utawala bora na maendeleo ya kikanda.
Ujumbe huo uliwakilishwa na Katibu Mkuu wa FP-ICGLR, Balozi Dkt. Deo Mwapinga, kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa ICGLR, Dkt. Mubita Luwabelwa. Katika ujumbe huo alikuwemo pia mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi Diana Chando.
Wakati wa mazungumzo hayo, washiriki walijadili fursa mbalimbali za ushirikiano kati ya Mwalimu Nyerere Foundation, ICGLR Regional Civil Society Forum na taasisi nyingine za kikanda katika kuendeleza amani, mshikamano na maendeleo endelevu katika Ukanda wa Maziwa Makuu.


Mkurugenzi wa Idara ya Amani ya Afrika, ndugu Miraji Magai ( wa kwanza kulia waliokaa) katika mkutano wa kimkakati wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari, Migogoro, Ukatili na Ubaguzi jijini Arusha

WATANZANIA KUNUFAIKA NA MAZUNGUMZO YA WAZEE KUHUSU AMANI, UMOJA NA HAKI
Watanzania wanatarajiwa kunufaika na juhudi za kuimarisha amani, umoja na haki kufuatia kufanyika kwa mkutano wa wazee uliopewa jina “Mazungumzo ya Wazee Kuhusu Amani, Umoja na Haki”, uliofanyika jana katika Ukumbi Mkuu wa The Mwalimu Nyerere Foundation na kuandaliwa na The Mwalimu Nyerere Foundation.
Katika mkutano huo, wazee walijadili kwa kina sababu zilizosababisha machafuko yaliyojitokeza siku ya uchaguzi, wakibainisha kuwa changamoto za mawasiliano, ukosefu wa mazungumzo ya wazi na uelewa mdogo wa haki za raia vimekuwa vikiathiri amani na mshikamano wa jamii, hali inayowaathiri moja kwa moja wananchi katika maisha yao ya kila siku.
Wazee walikubaliana juu ya haja ya kuimarisha utamaduni wa mazungumzo, umoja na haki kama njia ya kulinda maslahi ya Watanzania, wakisisitiza kuwa amani ya kudumu itawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa kwa haki, utulivu na mshikamano.



